Saturday, July 4, 2015

MAELEZO ZAIDI KUHUSIANA NA HUDUMA ZA SUCCESS LIVING TANZANIA



SUCCESS C LIVING NI NINI?
Success C Living ni huduma mahususi inayotoa mafunzo maalum na ushauri pia msaada wa kibiashara kwa wafanyabiashara wadogo wadogo na wale walio na hurka ya kufanya biashara. Mafunzo hayo yanalenga kumsaidia mfanyabiashara kuzijua njia mbali mbali ambazo zitamuwezesha kufanikiwa kibiashara na misaada itasaidia katika kujenga biashara.
HISTORIA YA SUCCESS C LIVING.
Huduma hii imeanzishwa mwaka 2011 na kampuni ya Made’Gene Inc. ya nchini Afrika kusini kwa lengo la kusaidia kampeni nzima ya “Tokomeza umasikini Afrika”. Success Living ni huduma na sio kampuni. Huduma imesambaa katika ukanda mzima wa kusini mwa Afrika na sasa Afrika mashariki.
Miaka 5 ya huduma bora.
MLENGWA NI NANI?
Mlengwa ni kila mtu mwenye nia ya kufanya biashara yenye mafanikio au ni mfanyabiashara mdogo mwenye uhitaji wa kufanikiwa katika biashara yake. Mafunzo yatakayotolewa yatakupa uelewa na akili ya biashara ambayo itakuwezesha kufanikiwa kibiashara.
WEWE NI MLENGWA?
Je, unafikiri huduma yetu itakufaa? Kama ndiyo,        Success C Living inakualika kuwa mwanachama utakaepewa mafunzo na huduma ziada mbali mbali ikiwemo misaada, mikopo, vitabu vitavyokupa uelewa zaidi wa mafunzo yatakayotolewa na kukufaidisha mbeleni katika biashara yako hata ushauri wa papo kwa hapo hadi miezi 6 mfululizo.
.
KAMA MWANACHAMA, UTAPATA MAFUNZO KWA MUDA GANI?
Mafunzo yataanza mara baada ya watu 20 na zaidi katika eneo lako kuthibisha kujiunga. Baada ya mafunzo kuanza, yatachukua muda wa wiki 3 mfululizo, siku 2 kwa kila wiki 1 sawa na siku 6 hadi mafunzo kumalizika. Baada ya hapo itakuwa ni wakati wa mwanachama wa Success C Living kutendea kazi kile atakachokuwa amekipata katika mafunzo. Success C Living itaendelea kuwa na wanachama wake hata baada ya mafunzo kumalizika kwa ajili ya kutoa huduma ziada kama ushauri na mikopo pia usimamizi wa biashara zitakazokua zinafanywa na wanachama, Huu ni muda wako, ni msimu wako, ni mwaka wako wa mabadiliko. Tengeneza maisha yako ya mbele.

KUNA GHARAMA ZOZOTE ZA KUJIUNGA AU HUDUMA?
Hakuna gharama zozote za kujiunga na huduma hizi. Kujiunga ni BURE kabisa. [Soma maelezo ya namna ya kujiunga na huduma hii]
Huduma zitakazotolewa ndizo zitakazolipiwa. Gharama hizo zitakuwa kwa ajili ya mishahara na posho kwa walimu watakaokuwa wanafanya kazi ya kutoa mafunzo pia huduma katika eneo husika, kubadili gharama zitakazokuwa zimetumika katika kutengeneza vitabu na vipeperushi saidizi kwa ajili ya kusaidia zoezi zima pia kumfanya mwanachama kutambua uchungu wa gharama alizotoa ili aweze kufanya vyema katika biashara yake.
Gharama hizo pia zitawezesha kusaidia walimu katika usafiri wa maeneo watakayokuwa wakifanyia kazi kwani maeneo mengi ni ya vijijini, mbali na pia usafiri mgumu. Ni motisha kwa walimu.

ITAGHARIMU KIASI GANI?
Baada ya kujiunga bure na huduma hizi, kila mwanachama atalipia kiasi fulani. Kiasi hicho kitatumika kama kilivyoelezewa awali. Kiasi kidogo cha ziada kitapelekwa katika vituo vya watoto yatima, mahospitalini na pia kununua chakula na mahitaji mbali mbali kwa ajili ya maeneo hayo.
Gharama hizo ni kama ifuatavyo:
*Darasa la mafunzo            tsh12,000/
  Kitambulisho                       tsh6,000/
  Huduma kwa mwezi         tsh10,000/
*Vipeperushi                        tsh5000/
Sehemu zenye alama ya nyota (*) ni lazima zilipiwe. Kitambulisho kitakuwezeshesha kuingia katika darasa lolote la mafunzo haya mahala popote pale nchini.
Huduma kwa mwezi utalipia kama utakuwa mwanachama wa muda mrefu (Miezi 6) wa Success Living Services.

FAIDA ZA HUDUMA HII NI ZIPI?
ü  Usimamizi bora wa biashara yako hadi miezi 6, ikiwa na maana kila utakapopatwa na shida katika biashara, Success Living itakuepo kutoa msaada.
ü  Misaada katika majanga mbali mbali kama kufiwa na ajali. Pale mwanachama [wa muda mrefu] atakapopatwa na janga lolote kwa bahati mbaya, Success Living itakuepo kusaidia.
ü  Mikopo midogo midogo. Ni kwa wanachama wa muda mrefu pia watakaokidhi vigezo na masharti watasaidiwa mikopo ili kusaidia biashara na maisha yao.
ü  Cheti cha mahudhurio kwa ajili ya biashara yako. Cheti hiki kitakusaidia wewe kuaminika zaidi na wateja wako kwa biashara bora na yenye bidhaa na huduma bora. Na faida nyingi nyinginezo…

UNAJIUNGAJE NA HUDUMA HII?
Ni rahisi sasa kujiunga, simu yako ya mkononi itakurahisishia kila kitu. Tuma ujumbe mfupi wa maneno wenye jina lako lote, kata, wilaya na mkoa unaoishi kwenda namba 0 7 6 8  9 6 6  6 8 1 na maswali kadhaa rahisi utatumiwa na utayajibu kwa njia hiyo. Au jaza fomu utakayopewa na agenti wetu na umkabidhi. Fomu ni BURE.


SUCCESS LIVING ITAHUDUMIA WATU CHINI YA 70 TU KWA KILA ENEO, HIVYO, WAHI NAFASI YAKO.

Tafadhali lipia huduma siku ya kwanza ya mafunzo, ogopa matapeli watakaokutoza kabla. Taarifa ya eneo la mafunzo litatangazwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno (SMS) pia walimu na maagenti wetu. Kama hutaweza kujiunga kwa wakati, karibu katika darasa la mafunzo na utapewa fomu ya kujiunga BURE.

Sunday, May 3, 2015

SuccessLiving Africa ni nini?

SuccessLiving ni kampeni ilioanzishwa tangu mwaka 2012 nchini Afrika ya kusini kwa ajili ya lengo la kusaidia waafrika kupambana na umaskini. Kampeni hii ya SuccessLiving Africa inasimamiwa na taasisi washirika mbalimbali ambao huendesha shule kadha wa kadha katika nchi kama Afrika ya kusini, Botswana, Zambia, Congo Brazzaville, Kenya na sasa Tanzania.

Lengo la SuccessLiving ni nini?

Lengo kuu la kampeni hii, SuccessLiving Afrika, ni kuifanya Afrika sehemu salama ya kuishi. Kampeni inaendesha shule mbali mbali zinazofundisha njia mbalimbali zinazoweza kutumika kupambana na umaskini, njia kuu ambayo imependekezwa na watu wengi katika nchi zilizotembelewa ni ‘biashara’. Biashara ndogo ndogo kwa kubwa, SuccessLiving inafundisha na kuhakikisha mlengwa anaondokana nao.


SuccessLiving wanafanyeje kazi?
 
SuccessLiving Africa inaendesha masomo ya kibiashara kwa wanachama tu. Hii itasaidia waendeshaji wa kampeni kuwa karibu zaidi na walengwa pia kuhakikisha walengwa wanapata msaada uliokamilika kuwasaidia kuondokana na umaskini. Ni rahisi kuwa mwanachama, fomu imeambatanishwa.

Faida za uanachama ni zipi? 

Kila mwanachama atasaidiwa kikamilifu kuondokana na umaskini na walimu waliobobea katika fani ya biashara pia maendeleo vijijini. Kama mwanachama, utakua na uwezo wa kuomba msaada wa kiushauri, kimkopo ama kiutendaji kwa walimu wako popote pale nchini kwani uanachama wako utakua ki-elektroniki. Kama mwanachama utapewa kitambulisho ambacho kitakuruhusu kuingia katika darasa lolote la mafunzo linalosimamiwa na SuccessLiving pia kitakua na namba ambao itasajiliwa ki-electroniki kumruhusu mwanachama kutambulika popote pale nchini.
Nimechagua SuccessLiving, Naishi na maendeleo pia mafanikio. Jiunge nami leo ujionee mwenyewe.


Kampeni hii imesaidia watu wengi sana katika nchi zilizotembelewa na kampeni hii, sasa ni wakati wako wewe kubadilisha maisha yako. Jiunge nasi leo!!