Sunday, May 3, 2015

SuccessLiving Africa ni nini?

SuccessLiving ni kampeni ilioanzishwa tangu mwaka 2012 nchini Afrika ya kusini kwa ajili ya lengo la kusaidia waafrika kupambana na umaskini. Kampeni hii ya SuccessLiving Africa inasimamiwa na taasisi washirika mbalimbali ambao huendesha shule kadha wa kadha katika nchi kama Afrika ya kusini, Botswana, Zambia, Congo Brazzaville, Kenya na sasa Tanzania.

Lengo la SuccessLiving ni nini?

Lengo kuu la kampeni hii, SuccessLiving Afrika, ni kuifanya Afrika sehemu salama ya kuishi. Kampeni inaendesha shule mbali mbali zinazofundisha njia mbalimbali zinazoweza kutumika kupambana na umaskini, njia kuu ambayo imependekezwa na watu wengi katika nchi zilizotembelewa ni ‘biashara’. Biashara ndogo ndogo kwa kubwa, SuccessLiving inafundisha na kuhakikisha mlengwa anaondokana nao.


SuccessLiving wanafanyeje kazi?
 
SuccessLiving Africa inaendesha masomo ya kibiashara kwa wanachama tu. Hii itasaidia waendeshaji wa kampeni kuwa karibu zaidi na walengwa pia kuhakikisha walengwa wanapata msaada uliokamilika kuwasaidia kuondokana na umaskini. Ni rahisi kuwa mwanachama, fomu imeambatanishwa.

Faida za uanachama ni zipi? 

Kila mwanachama atasaidiwa kikamilifu kuondokana na umaskini na walimu waliobobea katika fani ya biashara pia maendeleo vijijini. Kama mwanachama, utakua na uwezo wa kuomba msaada wa kiushauri, kimkopo ama kiutendaji kwa walimu wako popote pale nchini kwani uanachama wako utakua ki-elektroniki. Kama mwanachama utapewa kitambulisho ambacho kitakuruhusu kuingia katika darasa lolote la mafunzo linalosimamiwa na SuccessLiving pia kitakua na namba ambao itasajiliwa ki-electroniki kumruhusu mwanachama kutambulika popote pale nchini.
Nimechagua SuccessLiving, Naishi na maendeleo pia mafanikio. Jiunge nami leo ujionee mwenyewe.


Kampeni hii imesaidia watu wengi sana katika nchi zilizotembelewa na kampeni hii, sasa ni wakati wako wewe kubadilisha maisha yako. Jiunge nasi leo!!